MRIPUKO WA BOMU WAUWA WATANO-IRAQ:
6 Desemba 2003Matangazo
BAGHDAD: Mwanajeshi mmoja wa Kimarekani na Wairaqi wanne wamefariki kutokana na mripuko wa bomu lililotegwa kando ya barabara mjini Baghdad.Wengine 16 wamejeruhiwa.Bomu hilo liliripuka katika barabara inayotumiwa sana, ulipopita msafara wa wanajeshi na basi dogo lililojaa abiria.Shambulio hilo limetokea wakati ambapo Marekani imetoa wito kwa Shirika la Kujihami la Magharibi-NATO,kupeleka vikosi vyake nchini Iraq-hatua ambayo inapingwa na waziri wa ulinzi wa Ujerumani Peter Struck.Kwa upande mwingine mjini Washington Rais George W.Bush ametangaza uteuzi wa James Baker kama "mjumbe wake binafsi" kuongoza juhudi za kuijenga Iraq na kupunguza madeni yake ya kigeni.Baker ambae hapo zamani alikuwa waziri wa kigeni wa Marekani ni rafiki wa familia ya Bush.