MRIPUKO WA BOMU-IRAQ:
1 Januari 2004Matangazo
BAGHDAD: Si chini ya watu 5 wameuawa mjini Baghdad,katika mripuko wa bomu lililotegwa kwenye gari,nje ya mkahawa uliojaa watu waliokuwa wakisheherekea mwaka mpya.Yasemekana mkahawa huo unaotembelewa zaidi na wageni pamoja na Wairaqi wenye uwezo wao,umeharibiwa vibaya.Watu wengine 20 pia wamejeruhiwa.Miongoni mwao ni Mmarekani 1 na Waingereza 2.Gazeti la "Los Angeles Times" limearifu kuwa waandishi habari wake 3 na wafanyakazi 4 katika ofisi ya gazeti hilo mjini Baghdad walijeruhiwa,lakini hawamo katika hali ya hatari.Shambulio la jana usiku limetokea ingawa polisi wa Kiiraqi na vikosi vya muungano vilioikalia Iraq vimeimarisha usalama,baada ya kuwepo vitisho kuwa wanamgambo watashambulia wakati wa mapumziko ya mwaka mpya.