Wanawake wa eneo la Nandi wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kuja pamoja na kuimarisha biashara yao ya maziwa. Mafunzo ya usimamizi wa ng'ombe na kilimo cha nyasi za kisasa zinazoimarisha afya ya mifugo vimewabadilishia maisha. Mwandishi wa DW Kiswahili Thelma Mwadzaya alitembelea eneo hilo la Magharibi mwa Kenya.