Mpango wa Umoja wa Ulaya kuiadhibu Israel wakwama
15 Agosti 2025Wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya wameiambia DW kuwa Ujerumani ni miongoni mwa nchi waliotaka kuwepo muda zaidi wa kulipitia upya pendekezo hilo.
Mtendaji Mkuu wa Umoja wa Ulaya ameonya kuwa mateso ya kibinaadamu huko Gaza yamefikia viwango visivyofikirika, huku baa la njaa likijitokeza mbele ya macho yao. Mwishoni mwa mwezi Julai, katika juhudi za kuishinikiza Israel kubadili mwelekeo wake, Umoja wa Ulaya ulipendekeza kuzizuia kampuni changa za kiteknolojia za Israel kupata sehemu ya ufadhili wa utafiti unaojulikana kama ''Horizon Europe''. Hiyo iliashiria mabadiliko katika mtazamo wa umoja huo; ambapo kwa mara ya kwanza ulichukua hatua.
Palestina yaulaani mpango wa makaazi wa Israel
Katika pendekezo hilo la Julai, 28, Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya iliandika: ''kutokaa na uvamizi wake katika Ukanda wa Gaza na janga la kiutu lililofuatia, ikiwemo pamoja na vifo vya maelfu ya raia na kuongezeka kwa kasi idadi ya watu wenye utapiamlo uliokithiri hasa kwa watoto, Israel inakiuka haki za binadamu na sheria za kibinaadamu na hivyo inakiuka kanuni muhimu ya ushirikiano kati ya Umoja wa Ulaya na Israel''.
Awali, Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Maxime Prevot aliipanga Agosti 13 kama tarehe inayowezekana ya kupitishwa pendekezo hilo iwapo makubaliano yatafikiwa, lakini vyanzo vya Umoja wa Ulaya viliiambia DW kwamba palikuwepo na mabadiliko madogo wakati wa mkutano wa mawaziri wa umoja huo uliofanyika kwa njia ya mtandao siku ya Jumatatu.
Mpango wa EU lazima upate wingi wa nchi zenye sifa za umoja huo ili kupita
Ili kupita, mpango wa Umoja wa Ulaya unahitaji kile kinachojulikana kama wingi wa nchi zenye sifa za umoja huo wenye nchi wanachama 27, mfumo ambao maoni ya nchi zenye watu wengi ndiyo yana uzito zaidi. Wizara ya mambo ya nje ya Israel imeliita pendekezo hilo la Brussels la kuzuia fedha kuwa ''la kusikitisha,'' na kudai kuwa hatua zozote kama hizo za kuiadhibu zitatumika tu kuliimarisha kundi la Hamas, jambo ambalo Umoja wa Ulaya umelikanusha.
WAFA: Wapalestina 89 wauawa Gaza
Kukwama kwa pendekezo hilo kumeibua gadhabu kutoka kwa wanaharakati na mashirika ya kutetea haki za binaadamu, ambao kwa muda mrefu wameushutu Umoja wa Ulaya kwa kushindwa kutumia uwezo unaowezekana. Afisa wa Shirika la Kimataifa la Misaada la Oxfam, Bushra Khalidi, ameiambia DW kuwa ukweli kwamba Umoja wa Ulaya hauwezi kukubaliana katika hatua ndogo kama hiyo, ni fedheha.
Tangu shambulizi la Hamas Oktoba 7, 2023, Umoja wa Ulaya umekuwa na umoja katika kulilaani kundi hilo la wanamgambo, linalotambuliwa kama kundi la kigaidi na umoja huo, pamoja na kutoa wito wa kuachiwa mateka wa Israel. Lakini hapo ndipo umoja huo umeishia. Kila neno katika kila taarifa kuhusu uhusiano wa Ulaya na Israel limejadiliwa vikali tangu wakati huo.
UN yaiomba Israel kusitisha mpango wa kuukalia kimabavu Ukanda wa Gaza
Ujerumani kwa upande mwingine inajiona kuwa na jukumu la kihistoria kuelekea usalama wa Israel, kutokana na utawala wa Kinazi huko nyuma na mauaji ya kimfumo ya Wayahudi milioni sita wakati wa mauaji dhidi ya Wayahudi. Hata hivyo, wiki iliyopita, Kansela Friedrich Merz alitangaza kuwa Ujerumani itasitisha sehemu ya mauzo ya silaha kwa Israel, kwa kuhofia kuwa jeshi la Israel linaweza kuzitumia katika Ukanda wa Gaza, hatua inayoashiria mabadiliko ya ukosoaji wake.
Umoja wa Ulaya umesema kipaumbele chake ni kuhakikisha misaada inaingia Gaza wakati ambapo mzozo wa kibinaadamu unazidi kuongezeka. Na baada ya vitisho vya vikwazo, umoja huo ulitangaza kile kinachoonekana kuwa mafanikio mwezi uliopita.