Mpango wa kuudhibiti Ukanda wa Gaza hautofanikiwa
10 Februari 2025Matangazo
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya mapinduzi ya Iran mjini Tehran, al-Hayya alisema kwamba watapambana na mpango huo na kuhakikisha umeshindwa kama vile ilivyoshindwa mipango mingine ya awali.
Hapo jana, Trump alisema kuwa amejitolea kununua na kuudhibiti ukanda wa Gaza lakini anaweza kuruhusu tu sehemu za eneo hilo lililoharibiwa na vita kujengwa upya na mataifa mengine katika Mashariki ya Kati.
Haya yanajiri huku kundi hilo la wanamgambo likisema leo kuwa mmoja wa wapiganaji wake ameuawa na jeshi la Israel katika Ukingo wa Magharibi.
Wizara ya afya ya Palestina imesema mwanamume huyo wa umri wa miaka 20 aliuawa wakati wa operesheni ya kijeshi ya Israel katika kambi ya wakimbizi ya Nur Shams.