Mpango wa kuendeleza vita Gaza wapigwa Tel Aviv
10 Agosti 2025Matangazo
Maandamano hayo yaliandaliwa na jukwaa la familia za mateka walio Gaza kwa hofu kuwa operesheni za kijeshi zinazopangwa na Israel zitahatarisha maisha ya wapendwa wao.
Siku ya Ijumaa Baraza la Usalama la Taifa likiongozwa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu liliidhinisha mpango wa kuendeleza mashambulizi na kuuteka mji wa Gaza, ambao ndio mkubwa zaidi kwenye ardhi hiyo ya Wapalestina iliyoharibiwa na vita, kwa lengo la kuchukua udhibiti wa ukanda wote wa pwani.
Israel inaamini kuwa mateka bado wanazuiliwa katika maeneo ambayo hayako chini ya udhibiti wake, yakiwemo maeneo ndani ya Jiji la Gaza. Aidha Israel inakadiria kuwa mateka 50 bado wanashikiliwa na Hamas, na takriban 20 kati yao wanadhaniwa kuwa bado wako hai.