Elimu haina mwisho, ni mradi maalum wa kuwasaidia wasichana Tanzania, ambao hawajamaliza kidato cha nne, waliositisha masomo kwa sababu mbalimbali, ikiwemo ya kupata ujauzito, ufukara ndani ya familia au kuugua kwa muda mrefu. Mradi huu unaratibiwa na Wizara ya Elimu nchini humo.