Moto waripuka Uturuki
20 Agosti 2006Matangazo
ANKARA:
Moto mkubwa umeripuka huko kaskazini-mashariki mwa Uturuki kwenye sehemu ya bomba linalotumiwa kupitishia gesi kutoka Iran.Wakuu huko wamesema shehena ya gesi imesita na wazimamoto wanapigana kupambana na moto huo.Wanaarifu zaidi kwamba njama ya uharibifu yamkini ndio sababu.Waasi wa kikurdi-Kurdistan wokers Party-wanaendesha harakati zao katika eneo hilo.