Moto walikumba eneo la kusini mashariki mwa Ujerumani
3 Julai 2025Matangazo
Moto huo ulioanza kwenye kambi ya zamani ya mafunzo ya kijeshi katika jimbo la Saxony, sasa unaripotiwa kufika kwenye jimbo la Bradenburg, ambalo linauzunguka mji mkuu, Berlin.
Jioni ya jana, wakaazi wa kijiji kimoja kinachokaliwa na watu wenye ulemavu wa kudumu waliamriwa kuondoka, kwa mujibu wa mamlaka za zimamoto.
Masaa machache baadaye, wakaazi wa mji wa jirani nao pia walipokea ujumbe wa simu za mkononi kuwataka kuhama mara moja.
Hatua ambayo ililihusu eneo zima la Zeithain kufikia usiku wa manane kuamkia leo.
Kwa mujibu wa maafisa wa zimamoto, tayari hekta 600 zimeshaathirika kwa moto huo, lakini hakuna taarifa yoyote ya vifo wala majeruhi.