Moto wa nyika waendelea kurindima mashariki ya Ujerumani
4 Julai 2025Matangazo
Moto huo wa nyika katika eneo la Gohrischheide, mpakani mwa majimbo ya Saxony na Bradenburg, unazidi kusonga mbele.
Moto huo ulioanza siku ya Jumanne kwenye kambo ya zamani ya mafunzo ya kijeshi, umekuwa shida kudhibitiwa kutokana na upepo mkali na pia ardhi ya eneo hilo kuwa na baruti nyingi zinazoripuka.
Afisa mkuu wa eneo hilo, Ralf Hänsel, amesema kiwango cha moto huo hakifahamiki, lakini baadhi ya wazimamoto wameliambia shirika la habari la Ujerumani, dpa, kwamba wanakisia hekta 1,000 zimeathiriwa.
Serikali imeongeza idadi ya wazimamoto kutoka 200 hadi 500, lakini hakuna uhakika wa lini watakamilisha udhibiti wa moto huo. Hali ya hatari imetangazwa na watu kwenye manispaa mbili na mji mmoja wametakiwa kuhama makaazi yao haraka.