Moto katika duka kubwa Iraq waua watu 61
17 Julai 2025Moto uliozuka katika jengo kubwa la maduka katika mji wa mji wa Kut mashariki mwa Iraq umewaua watu wapatao 60, huku familia zilizojawa na huzuni zikiendelea kuwatafuta jamaa wao ambao hawajulikani waliko.
Takribani watu wawili wameliambia shirika la habari la AFP kwamba wamewapoteza jamaa zao watano ambao walikuwa wamekwenda katika jumba hilo jipya la maduka linalojumuisha pia mgahawa la Hyper Mall lililofunguliwa hivi majuzi.
Maafisa wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo, huku waokoaji wakiendelea kuwatafuta watu ambao hawajulikani waliko.
Wizara ya mambo ya ndani imesema katika taarifa yake kwamba moto huo umewaua raia 61 wasio na hatia, wengi wao wakifa kwa kushindwa kupumua bafuni na kati yao miili 14 iliyoungua bado haijatambuliwa.