MOSUL: Wanamgambo waendelea kushambulia nchini Iraq
26 Juni 2005Matangazo
Mashambulio ya kujitolea muhanga maisha yameutikisa mji wa Mosul kaskazini mwa Iraq.Hadi watu 26 waliuawa katika mashambulio matatu mbali mbali.Shambulio moja lilifanywa dhidi ya kituo cha ukaguzi cha jeshi la Iraq kaskazini-mashariki mwa Mosul.Na katika mji wa Mosul,wanamgambo walishambulia makao ya polisi na hospitali kuu ya Mosul.Tawi la mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda nchini Iraq,limesema kuwa limehusika na mashambulio mawili ya kwanza.Wanamgambo wanaojaribu kuleta vurugu nchini Iraq,hulenga vikosi vya usalama nchini humo.