Mosko: Waasi wa Chechnia walilripua gari la polisi. Watu 12 wamuwawa
19 Julai 2005Matangazo
Si chini ya watu 12 wameuliwa huko Chechnia baada ya waasi kulishambulia gari ya polisi. Mashirika ya habari ya Russia, ITAR-Tass na RIA-Navosti, yakizinukulu idara za usalama, yalisema mripuko huo ulitokea katika wilaya ya NADTERECHNY katika Jamhuri ya Chechnia inayotaka kujitenga, kilomita 60 kutoka mji mkuu wa Grozny. Wiki iliopita Rais Vladimir Putin aliutembelea mkoa wa Dagestan, ulio jirani na Chechnia, ambako aliwataka mawaziri na makamanda wa jeshi wazidishe juhudi zao za kuzuwia michafuko.