MOSCOW:Putin akutana na afisa wa nulkea wa Iran
19 Februari 2005Matangazo
Rais Vladimir Putin was Russia amesema ana imani kwamba Iran haina nia ya kutengeneza silaha za nuklea.
Hata hivyo ameonya kwamba serikali ya Iran lazima iheshimu vikali sheria kuhakikisha kwamba haifanyi hivyo katika msaada inayopatiwa na Russia kwa mipango yake ya kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za nuklea.Putin alikuwa akizungumza na mjumbe wa ngazi ya juu wa Iran katika masuala ya nuklea Hassan Rowhani mjini Moscow.
Serikali ya Marekani imeishutumu Russia kwa kuendelea na mpango wake wa kujenga mtambo wa nuklea huko Bushehr kusini mwa Iran.Marekani imekuwa ikishutumu Iran kwa kutaka kujipatia silaha za nuklea.
Iran yenyewe imekuwa ikisisitiza kwamba mpango wake huo wa nuklea ni kwa ajili ya dhamira za amani tu.