MOSCOW: Rice ashindwa kuishawishi Urusi juu ya Iran
16 Oktoba 2005Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani bibi Condoleeza Rice ameshindwa kuishawishi Urusi juu ya kuwa na msimamo mkali dhidi ya Iran kutokana na mpango wa nyuklia wa nchi hiyo.
Mrekani inataka kuifikisha Iran mbele ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ikiwa nchi hiyo itaendelea na mpango wake wa nyuklia na ikiwa itaendelea kukataa kufanya mazungumzo juu ya suala hilo.
Lakini Urusi imesema suala hilo linapaswa kuzingatiwa na shirika la kimataifa la udhibiti wa nishati ya nyuklia.
.