MOSCOW: Putin aiunga mkono Ujerumani kuwa na kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama
7 Mei 2005Matangazo
Rais Vladimir Putin wa Russia amesema anaiunga mkono Ujerumani katika juhudi yake ya kugombea kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Katika mahojiano pamoja na gazeti la Kijerumani “Bild”, Putin amesema Russia itaiunga mkono Ujerumani iwe na dhima imara katika Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na kuwa na kiti cha kudumu kwenye Baraza la Usalama.Jumatatu ijayo mjini Moscow,Rais Putin na Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani watahudhuria pamoja sherehe ya kutimiza miaka 60 tangu kumalizika kwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.