MOSCOW Putin aadhimisha uvamizi wa muungano wa Kisovieti na wanajeshi wa Ujerumani
22 Juni 2005Matangazo
Rais wa Russia, Vladamir Putin, ameweka shada la maua kwenye kaburi la mwanajeshi mmoja asiyejulikana mjini Moscow, katika maadhimisho ya miaka 64 tangu manazi wa Ujerumani walipouvamia muungano wa Kisovieti.
Mwezi Mei mwaka huu, wanasiasa mashuhuri ulimwenguni kote walikusanyika mjini Moscow kuadhimisha miaka 60 ya ushindi wa jeshi la muungano dhidi ya wanajeshi wa Ujerumani wakati wa vita vya pili vya dunia. Zaidi ya raia milioni 27 wa Urusi ya zamani waliuwawa katika vita hivyo.