MOSCOW Iran haina mpango wa kutengeneza silha za kinuklia.
18 Februari 2005Rais wa Urusi, Vladamir Putin, amesema anaamini kwamba Iran haina mpango wowote wa kutengeneza silaha za kinuklia, na akaahidi kuendeleza uhusiano wake wa nishati ya nuklia na taifa hilo la kiislamu. Hata hivyo Putin amemwambia mpatanishi mkuu wa Iran wa swala la nishati ya nuklia, Hassan Rohani, katika mazungumzo yao kwenye ikulu ya Kremlin, kwamba anatumai serikali ya Tehran itatimiza makubaliano kati yake na Urusi na jamii ya kimataifa. Marekani imeilaumu serikali ya Moscow kwa kuendeleza shughuli za ujenzi wa kiwanda cha nishati ya nuklia huko Bushehr, kusini mwa Iran. Serikali yaWashington ina wasiwasi huenda Iran inatumia ujuzi wa Urusi kutengeneza silaha za kinuklia. Iran imeiunga madai hayo, ikisisitiza inataka nishati ya nuklia kwa kuzalisha umeme.