MORONI: Upinzani kuitisha maandamano zaidi-
2 Desemba 2003Matangazo
Vyama vya upinzani katika visiwa vya Comoros, vimesema vitaitisha maandamano zaidi, ya kumtaka Rais wa visiwa hivyo Azali Assoumani aondoke madarakani.
Tangazo la muungano wa vyama vyote vya upinzani visiwani Comoros, lililotokewa leo asubuhi, linasema lazima Rais Azali Assoumani aheshimu aliyoahidi wananchi au anga'atuke.
Chama kikuu cha upinzani RIDJA, kiliitisha maandamano makubwa mwezi September uliopita, ya kupinga ughali wa maisha visiwani Comoros, ambayo yalisababisha machafuko makubwa na kupelekea kiongozi wa chama hicho Said Larifou kutiwa mbaroni.
Watu kumi na watano walijeruhiwa katika maandamano yaliyofanyika tarehe ishirini na sita mwezi November uliopita, ambapo wanajeshi walibidi kutumia gezi za kutoa machozi, na kufyatua risasi, ili kutawanya waandamanaji.