Morocco na Madagacar kukutana katika fainali za CHAN
27 Agosti 2025Matangazo
Mabingwa watetezi, Senegal, walitangulia kufunga kupitia kwa mchezaji Joseph Layousse, lakini dakika saba baadaye Moroko walijibu kupitia Sabir Bougrine.
Kwa kuwa mechi ilibaki sare ya 1-1 hadi mwisho wa muda wa nyongeza, penalti zikaamua mshindi.
CHAN: Sudan, Madagascar, Morocco na Senegal zatinga nusu fainali
Matokeo haya yatawakutanisha mabingwa wa mwaka 2018 na 2020, Morocco dhidi ya Madagascar kwenye fainali siku ya Jumamosi jijini Nairobi, baada ya taifa hilo la kisiwa kuwafunga Sudan.
Sudan itakipiga na Senegal katika mechi ya mshindi wa tatu Ijumaa tarehe 29 katika uwanja wa Mandela nchini Uganda.