MOGADISHU: Gedi aomba msaada wa mafunzo ya polisi
28 Agosti 2006Matangazo
Waziri mkuu wa Somalia,Ali Mohamed Gedi ameomba msaada wa kigeni wa kutoa mafunzo kwa vikosi vya usalama vya serikali yake dhaifu inayozidi kukabiliwa na vitisho kutoka Muungano wa Kiislamu ulio na nguvu nchini mwake.Akizungumza katika sherehe ya kuadhimisha kuanza kwa mafunzo ya makuruta wapya wa polisi,Gedi alionya kuwa bila ya msaada wa kigeni,kuna hatari kuwa ukosefu wa utulivu utaendelea katika nchi hiyo kwenye Pembe ya Afrika.