Mtu mmoja auwawa wakati wa maandamano Nairobi
17 Juni 2025Matangazo
Kulingana na shirika la habari la Reuters, lilishuhudia mwili wa mtu aliyelala chini katika mji mkuu Nairobi akiwa na jeraha lililokuwa likivuja damu kichwani.
Soma zaidi: Polisi yatawanya maandano ya kupinga mauwaji ya mwalimu Kenya
Wakati wa maandamano hayo liliibuka kundi la wanaume waliobeba bakora na virungu wakiwa kwenye pikipiki ambao waliwashambulia waandamanaji. Awali polisi walifyatua mabomu ya machozi ili kuwatawanya waandamanaji katikati ya mji huo.
Waandamanaji hao wanamtaka Naibu mkuu wa Polisi Eliud lagat ajiuzulu kufuatia kifo cha kutatanisha cha Albert Ojwang. Lagat alitangaza kuondoka madarakani kwa muda ili kupisha uchunguzi wa kifo cha Albert.