Mmoja auawa na 10 wajeruhiwa katika shambulizi la Urusi
5 Agosti 2025Matangazo
Maafisa wa Shirika la Reli la Ukraine, Ukrzaliznytsia wamesema shambulizi hilo kubwa limeharibu kituo cha treni na miundombinu mingine kwenye mji huo, ambao ni kitovu cha usafiri katika jimbo la Kharkiv linalopakana na Urusi.
Meya wa Lozova, Sergiy Zelensky amesema watu kadhaa wamejeruhiwa wakiwemo watoto wawili, na nyumba za makaazi zimeharibiwa.
Watu wengine wawili pia wamejeruhiwa katika shambulizi tofauti la droni la Urusi kwenye jimbo la Zaporizhzhia.
Wakati huo huo, jeshi la anga la Ukraine limesema vitengo vyake vya ulinzi wa anga vimezidungua droni 29 chapa Shahed zilizotengenezwa Iran, usiku wa kuamkia Jumanne kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.