Mmoja ashikiliwa kwa kumchoma mtalii kwa kisu
22 Februari 2025Matangazo
Mamlaka zilisema baada ya tukio hilo kwamba inamshikilia mshukiwa huyo aliyekuwa karibu na eneo kulikofanyika tukio na ambaye alikuwa na madoa ya damu.
Gazeti la Tagesspiegel liliripoti kwamba kufuatia kisa hicho, polisi walilifunga jumba hilo la makumbusho ya Wayahudi waliouawa barani Ulaya na mtalii huyo alikimbizwa hospitalini ambako anatibiwa majeraha ambayo hata hivyo hayakuwa na kutishia maisha yake.