Mlipuko mpya wa Ebola nchini DRC umewaua watu 15
5 Septemba 2025Matangazo
Mamlaka ya afya katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imetangaza mlipuko mpya wa virusi vya Ebola, ambao tayari umesababisha vifo vya watu 15 tangu mwishoni mwa Agosti, Waziri wa Afya Samuel Roger Kamba alitoa taarifa hiyo Alhamisi. Kamba aliwaambia waandishi wa habari mjini Kinshasa kwamba mlipuko huo mpya umetokea katika Mkoa wa Kasai katikati mwa nchi. Kwa mujibu wa takwimu za awali, jumla ya visa 28 vinavyoshukiwa vimeripotiwa katika Mkoa wa Kasai, ambapo kisa cha kwanza kilikuwa cha mwanamke mjamzito mwenye umri wa miaka 34 aliyelazwa hospitalini tarehe 20 Agosti. Huo ni mlipuko wa 16 uliowahi kurekodiwa nchini humo ambapo wa mwisho ulitokea miaka mitatu iliyopita na ulisababisha vifo vya watu sita.