Mkuu wa UNHCR asema Kongo, Rwanda kuwarejesha wakimbizi
27 Agosti 2025Tamko hilo la Grandi akiwa mjini Kinshasa, limejiri wakati mivutano ikiendelea kati ya Kongo na Rwanda, licha ya kuwepo mpango wa amaniuliosimamiwa na Marekani ambao nchi hizo mbili jirani zilitia saini mwezi Juni.
Grandi, akizungumza na waandishi habari baada ya kukutana na Rais Felix Tshisekedi, amesema wakimbizi 533 wa Rwanda waliokuwa wakiishi nchini Kongo walirudishwa Rwanda katika kipindi cha siku mbili zilizopita, chini ya usimamizi wa shirika lake. Alizihimiza pande zote kuheshimu kanuni kwamba kurudi kwa Wakongo na Wanyarwanda ambao walikuwa wamehama makwao kutokana na machafuko mashariki mwa Kongo lazima "kuwe kwa hiari".
Shirika moja lisilo la kiserikali, la Human Rights Watch mwezi Juni lilishutumu kundi la waasi wa M23 kwa kuwafukuza kwa nguvu zaidi ya watu 1,500 kwenda nchini Rwanda, na kuishinikiza UNHCR kusaidia katika operesheni hiyo, jambo ambalo Kigali inakanusha.