Mkuu wa shirika la misaada kwa Gaza ajiuzulu
26 Mei 2025Matangazo
Mkurugenzi mtendaji wa Wakfu wa Kibinaadamu wa Gaza, Jake Wood, alisema siku ya Jumatatu (Mei 26) kwamba amelazimika kujiondosha kwenye nafasi yake baada ya kutambua kwamba shirika hilo haliwezi kutimiza majukumu yake kwa namna inayokwendana na misingi ya huduma za kibinaadamu.
Soma zaidi: Watu 22 wauwawa kwa mashambulizi ya Israel mjini Gaza
Shirika hilo, ambalo lina makao yake makuu mjini Geneva tangu mwezi Februari, lilikuwa limeazimia kusambaza milo milioni 300 katika miezi mitatu ya mwanzo ya operesheni yake huko Gaza.
Lakini Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa tayari yalishasema yasingelishirikiana nalo, huku kukiwa na tuhuma za kwamba linatumika na Israel.