Mkuu wa MONUSCO Bintou Keita afanya ziara Goma
13 Juni 2025Matangazo
Kulingana na taarifa ya MONUSCO iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa X, mwakilishi huyo maalum wa Umoja wa Mataifa anatarajiwa kukutana na wawakilishi wa muungano wa M23 na AFC, ambao unaudhibiti mji huo ulioko mashariki mwa Kongo.
Rwanda yajiunga na ukosoaji wa utawala mbadala wa M23
Mazungumzo baina ya pande hizo mbili yatajumuisha vipaumbele vya mamlaka ya MONUSCO, hasa ulinzi wa raia. Msemaji wa MONUSCO, Sakuya Oka amesema ziara ya Keita inafanyika kabla ya kutoa taarifa yake katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Juni 27.
Wakati huo huo, Marekani imezishinikiza Rwanda naKongokufikia makubaliano ya amani ndani ya mwezi huu wa Juni au mapema mwezi ujao.