UchumiKimataifa
IMF: Ushuru mpya wa Trump ni hatari kwa uchumi wa dunia
4 Aprili 2025Matangazo
Bi Georgieva amesema ni muhimu kuepuka vitendo vinavyoweza kudhuru zaidi hali ya uchumi wa dunia. Hatua hiyo ya Marekani imezusha hofu na ukosoaji mkubwa kote duniani huku nchi kadhaa zikisema kuwa tayari kulipiza kisasi.
Soma pia: IMF na Benki ya Dunia kuendelea kushirikiana na Trump
Trump amesema ushuru huo kwa bidhaa zinazoingia Marekani ni hatua ya kulipiza kile ambacho mataifa husika yamekuwa yakiifanyia Marekani kwa muda mrefu na kwamba unalenga kurejesha uzalishaji wa ndani na kulinda ajira za Wamarekani.