Mkuu wa IAEA Rafael Grossi kuelekea Tehran wiki hii
14 Aprili 2025Mkuu wa shirika la kudhibiti nguvu ya Atomiki duniani,la IAEA, Rafael Grossi amesema atakwenda Tehran wiki hii kabla ya duru ya pili ya mazungumzo ya Nyuklia kati ya Iran na Marekani.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Iran,Grossi anatarajiwa siku ya Jumatano mjini Tehran.
Soma pia: China na Urusi zaiunga mkono Iran wakati Trump akishinikiza mazungumzo ya nyukliaZiara ya Grossi Tehran inafanyika baada ya Jumamosi, Marekani na Iran kuanza mazungumzo mjini Muscat kuhusu uwezekano wa kupata makubaliano mapya ya Nyuklia.
Marekani na nchi za Magharibi zina wasiwasi na mpango wa nyuklia wa Iran kwamba sio wa amani. Vyanzo kutoka Italia, vimefahamisha kwamba mataifa hayo mawili yanatarajiwa kukutana kuendeleza mazungumzo hayo mjini Roma, mwishoni mwa juma.