SiasaIran
Mkuu wa IAEA Rafael Grossi afanya ziara mjini Tehran
17 Aprili 2025Matangazo
Kauli ya Grossi imetolewa wakati wajumbe wa Iran na Marekani wanatarajiwa kukutana mjini Roma, Jumamosi, kwa ajili ya duru ya pili ya mazungumzo baada ya kukamilika duru ya kwanza nchini Oman.
Mkuu huyo wa IAEA amesema alipokuwa ziarani mjini Tehran leo kwamba kwa sasa mazungumzo hayo yamefikia kwenye hatua muhimu licha ya muda kuwa mchache huku akiahidi kusaidia kuuwezesha mchakato huo.
Soma pia: Iran: Duru ya pili mazungumzo na Marekani itafanyika Roma
Itakumbukwa kuwa Rais wa Marekani Donald Trump aliyafuta makubaliano ya kihistoria ya nyuklia na Iran mnamo mwaka 2018.