SiasaMamlaka ya Palestina
Türk ashtushwa na mashambulizi ya Israel ukanda wa Gaza
18 Machi 2025Matangazo
Kulingana na Turk, hatua ya Israeli kutumia nguvu zaidi ya kijeshi itaongeza tu mateso zaidi kwa Wapalestina ambao tayari wanakabiliwa na hali mbaya iliyoko.
Soma pia: Makabidhiano ya miili ya mateka wa Israel yakosolewa
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema ameliambia jeshi kuchukuwa hatua kali dhidi ya Hamas kujibu hatua ya kundi hilo ya kukataa kuwaachia huru mateka waliosalia pamoja na mapendekezo ya kusitisha mapigano.
Ajith Sunghay, mkuu wa Ofisi ya Haki za Binadamu katika Ukanda wa Gaza, ametaja kuanza tena kwa mashambulizi hayo ya Israel kuwa hatua ya kutisha baada ya miezi miwili ya kusitishwa kwa mapigano.